TUME YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA ZANZIBAR
Tovuti ya huduma binafsi kwa viongozi
Sehemu salama ya kujisajili, kusasisha taarifa zako na kuwasilisha matamko yako.
Fuata Maadili, Tuimarishe Utawala Bora
Jisajili kama kiongozi
Wasilisha usajili wako na nyaraka zinazohitajika kwa mapitio.
Anza usajiliIngia kwenye akaunti
Endelea kwenye dashibodi, taarifa na matamko yako.
Ingia kwa usalamaMaelezo Muhimu
FOMU YA KUTANGAZA RASILIMALI, MAPATO, MADENI NA MATUMIZI
(Kwa Mujibu wa Kifungu cha 25 na 26)
Tafadhali soma kwa makini maelezo yanayofuata kabla ya kutoa Tamko la Rasilimali, Mapato, Madeni na Matumizi.
Kabla ya kujaza Fomu hii soma kwa makini kifungu cha 25 na 26 cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Nam.….. ya Mwaka 2026. Orodha ioneshe mali za kibiashara na za matumizi binafsi.
Orodhesha mali unazomiliki, mali za mke au mume wako, mali unazomiliki kwa pamoja na mtu yeyote, mali za watoto wenye umri ulio chini ya miaka kumi na nane ambao hawajaoa au kuolewa, Rasilimali ambazo uliwahi kumiliki na kuhaulisha au ulimnunulia mtu yeyote ndani ya kipindi cha Miaka Miaka Mitano, Rasilimali yeyote ambayo ipo chini ya uangalizi wako na Rasilimali yako ambayo ipo chini ya uangalizi wa mtu mwengine. Rasilimali, Mapato, Madeni na Matumizi yanayotakiwa kutajwa ni pamoja na:-
- Taarifa Binafsi za Kiongozi, Mume au Mke, Watoto na Washirika na Wasimamizi wa Mali za Kiongozi;
- Fedha taslimu, Fedha ambazo hazipo Benki ikiwemo Mitandao ya Simu, Saccoss, Vikoba na Amana katika Benki au Taasisi nyingine ya Fedha ndani na nje ya Zanzibar;
- Faida itokanayo na fedha iliyowekwa akiba katika Benki au Taasisi nyingine ya fedha;
- Mgao wa fedha au faida nyengine inayotokana na fungu la rasilimali ya kampuni au hisa za kiongozi wa umma katika kampuni, soko la hisa au shirika lolote;
- Hawala za Hazina (Treasury Bills) na nyinginezo za dhamana maalum zinazotolewa au kudhaminiwa na Serikali au vyombo vya Serikali;
- Maslahi katika chombo cha biashara kisichokuwa na mkataba na Serikali, na kisichokuwa au kisichodhibiti amana zinazouzwa bayana na vyombo vya umma; isipokuwa kwa dharura, na ambazo fungu lake la rasilimali na hisa haziuzwi bayana kwa umma;
- Viwanja, Mashamba na Ardhi zinazotumika kibiashara na ya matumizi binafsi;
- Mali zinazohamishika na zisizohamishika, ambazo zinamilikiwa na kusimamiwa kwa njia ya Uwakala;
- Mali zinazoleta faida zinazomilikiwa na kusimamiwa na kiongozi wa umma, mke/mume au watoto ndani na nje ya Zanzibar;
- Madeni yanayozidi kiwango cha mshahara kwa mwaka bila ya kujumuisha Maposho; na
- Matumizi ya kiongozi wa umma ndani ya kipindi cha mwaka anachotoa tamko.
Unapaswa kutaja Rasilimali zako mume/mke na watoto ikiwemo mali zinazohamishika na zinazohamishika. Pia orodhesha Mapato, Madeni na Matumizi yako pamoja akaunti na biashara unazomiliki kwa pamoja na mtu au watu wengine zilizoko ndani na nje ya Zanzibar.
Sehemu ya Rasilimali za Mume/Mke au Wake na Watoto ijazwe na Kiongozi wa Umma kwa ajili ya Mume/Mke au Wake,Watoto, Wasimamizi na Washirika wa Mali kwa kadri ilivyo.
Ambatanisha nakala zinazohitajika kwa mujibu wa Tamko.
Ni ukiukwaji wa Maadili kwa kiongozi wa umma kushindwa kuwasilisha Fomu ya Tamko la Rasilimali, Mapato, Madeni na Matumizi katika muda uliowekwa na Sheria. Ni kosa la jinai kutoa tamko na taarifa za uongo kuhusu Rasilimali, Mapato, Madeni na Matumizi yake.
Baada ya kuijaza kwa ukamilifu, Tamko hili liwasilishwe kwa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa njia ya kieletroniki ndani ya siku thelathini baada ya kushika wadhifa, kabla ya tarehe 31 Disemba ya kila mwaka na ndani ya miezi mitatu baada ya kumaliza au kuondoshwa katika nafasi ya uongozi au ajira
Ni wajibu wako kuhakikisha kwamba Fomu ya Tamko iliyokamilika imefika Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma kama ilivyoelekezwa katika kifungu cha 25 cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Zanzibar Nam…. ya mwaka 2026.
Fomu hii inapatikana katika Mfumo wa Kielektroniki wa Usajili wa Taarifa za Rasilimali, Mapato, Madeni na Matumizi ya Viongozi wa Umma.
Fomu hii itajazwa kikamilifu endapo Kiongozi wa Umma anajaza kwa mara ya kwanza, Kiongozi anaejaza fomu kwa mara nyingine atatakiwa kujaza taarifa za nyongeza, pungufu na mabadiliko ya taarifa binafsi, taarifa za rasilimali, mapato, madeni na matumizi.